Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wagalatia Utangulizi

Utangulizi
Paulo aliandika waraka huu katika safari yake ya kwanza kueneza Injili. Baada yake kuondoka Galatia, waumini Wayahudi walifika huko, nao wakaanza kusisitiza kwamba lazima watu wa Mataifa walioamini kwanza watimize Sheria ya Musa ili wapate kuokoka. Paulo aliandika kupinga mafundisho hayo, akionesha jinsi Abrahamu, ambaye aliishi miaka 400 kabla ya Sheria ya Musa kutolewa, alivyookolewa kwa imani. Alionesha kwamba kama vile Sheria haingeweza kumwokoa mtu, basi hakuna mtu angeweza kuwa mkamilifu kwa kujitahidi kwa uwezo wake mwenyewe kuitimiza Sheria.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kukataa mafundisho ya kuwa muumini wa Mataifa ni lazima atii sheria za Kiyahudi ndio aokolewe.
Mahali
Antiokia.
Tarehe
Mnamo 49 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Tito, Barnaba, Petro, na walimu wa uongo.
Wazo Kuu
Paulo anatetea kwa bidii kweli ya Injili ambayo kiini chake ni kwamba, “Mtu anaokolewa kwa neema ya Mungu kwa kumwamini Kristo.”
Mambo Muhimu
Paulo anasisitiza uhalali wa Injili, ubora wa Injili, na uhuru wa Injili.
Yaliyomo
Paulo atetea Injili na mamlaka yake kama mtume (1:1–2:21)
Kuwekwa huru kutokana na Sheria (3:1–4:31)
Uhuru wa Mkristo (5:1‑26)
Mawaidha kuhusu mwenendo wa Mkristo (6:1‑18).

Iliyochaguliwa sasa

Wagalatia Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia