Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezra Utangulizi

Utangulizi
Kitabu cha Ezra na Nehemia vilikuwa kitabu kimoja katika Biblia ya Kiebrania ambacho kilijulikana kama Ezra. Kitabu cha Ezra kinaelezea juu ya kurudi kwa Wayahudi kutoka uhamishoni Babeli. Kinaanzia 539 K.K. na agizo alilotoa Koreshi, mfalme wa Uajemi, linalotajwa katika milango miwili ya mwisho ya Mambo ya Nyakati, ambalo liliwaruhusu watu kurudi Yerusalemu chini ya uongozi wa Zerubabeli. Watu walianza kujenga Hekalu kwa hamu na juhudi kubwa, na wakaanza kutoa dhabihu. Lakini kwa miaka 18 walicheleweshwa na adui zao kutoka kaskazini. Hatimaye mnamo 521 K.K. agizo kutoka kwa Dario mfalme wa Uajemi liliwapa nafasi ya kumalizia ujenzi huo. Walikamilisha kazi hiyo na kuweka Hekalu wakfu mnamo 516 K.K.
Katika mwaka wa 458 K.K., Kuhani Ezra aliwasili Yerusalemu akiwa na kundi jingine la watu waliokuwa wamesalia uhamishoni huko Babeli. Aliwafundisha watu Sheria ya Mose, na akarekebisha maisha yao ya kiroho ili mataifa yaliyowazunguka waweze kuona kwamba hili ni taifa lililochaguliwa na Mungu.
Mwandishi
Kuna uwezekano mkubwa kwamba ni Ezra aliyeandika kitabu hiki.
Kusudi
Kuonyesha uaminifu wa Mungu, na vile aliweka ahadi yake kwa kuwarejesha watu wake katika nchi yao.
Mahali
Babeli na Yerusalemu.
Tarehe
Kitabu hiki kinadhaniwa kiliandikwa mwaka wa 450 K.K.
Wahusika Wakuu
Koreshi, Zerubabeli, Hagai, Zekaria, Dario wa Kwanza, Artashasta wa Kwanza, na Ezra.
Wazo Kuu
Kuweka kumbukumbu ya mkusanyiko wa kwanza wa Israeli kitaifa baada ya kutawanyika miongoni mwa mataifa; pia kuonyesha matatizo yanayoambatana na uhamisho wa kidini kuwiana na Sheria ya Mose.
Mambo Muhimu
Kurudi kwa Wayahudi kutoka uhamishoni. Kujengwa upya kwa Hekalu. Matatizo yaliyowakabili Waisraeli kutokana na kulijenga Hekalu la Mose.
Mgawanyo
Kikundi cha kwanza kinatoka uhamishoni Babeli na kurudi Yuda (1:1–2:70)
Kujengwa kwa Hekalu (3:1–6:22)
Kurudi kwa kikundi cha pili kutoka Babeli, pamoja na Ezra na huduma yake (7:1–10:44).

Iliyochaguliwa sasa

Ezra Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia