Ezra 2:64-70
Ezra 2:64-70 NENO
Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa elfu arobaini na mbili na mia tatu na sitini (42,360); tena zaidi ya hao walikuwa na watumwa wa kiume na wa kike elfu saba, mia tatu na thelathini na saba (7,337); pia walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake mia mbili. Walikuwa na farasi mia saba thelathini na sita (736), nyumbu mia mbili arobaini na watano (245), ngamia mia nne thelathini na watano (435), na punda elfu sita, mia saba na ishirini (6,720). Walipofika kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni elfu sitini na moja za dhahabu, mane elfu tano za fedha, na mavazi mia moja ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo. Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.