Ezekieli Utangulizi
Utangulizi
Kitabu hiki kimepewa jina la nabii Ezekieli ambalo maana yake ni “Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu”. Nabii Ezekieli alizaliwa katika jamii ya kikuhani na kulelewa katika mazingira ya Hekalu huko Yerusalemu. Mnamo mwaka wa 597 K.K., Ezekieli alikuwa mmoja wa mateka 10,000 waliopelekwa uhamishoni Babeli. Mwenyezi Mungu alimwita katika huduma mnamo mwaka wa 593 K.K., kupitia ufunuo.
Katika sehemu ya kwanza ya huduma yake, alitoa ujumbe kama ule Yeremia aliokuwa ameutoa kwamba mji wa Yerusalemu pamoja na Hekalu vingeliharibiwa. Wingi wa dhambi na ibada za sanamu zilizokuwa zikiendelea huko Yerusalemu kungesababisha Mwenyezi Mungu kuliacha Hekalu na Yerusalemu pia, kukifuatiwa na hukumu. Kwenda kwao Babeli, kutekwa na kuharibiwa kwa Yerusalemu ilikuwa ni uthibitisho.
Baada ya habari kufika Babeli mwaka wa 586 K.K. kwamba Yerusalemu ilikuwa imeangamizwa, Ezekieli alitoa ujumbe mpya wa matumaini ya kurejeshwa kwa Waisraeli. Kama Mchungaji Mkuu, Mwenyezi Mungu angewakusanya tena Waisraeli kutoka miisho ya dunia na kuwaimarisha tena katika nchi yao wenyewe. Mataifa ambayo yangeleta upinzani kuhusu kurejea kwa Waisraeli yangeshindwa na kuhukumiwa.
Mwandishi
Ezekieli mwana wa Buzi.
Kusudi
Kuwaonya watu juu ya dhambi na kutokutii kwao. Pia, kuonesha wema wa Mwenyezi Mungu kwa watu wake na kuweka wazi rehema za Mwenyezi Mungu endapo wangetubu.
Mahali
Babeli.
Tarehe
Mnamo 590–571 K.K.
Wahusika Wakuu
Ezekieli, viongozi wa Israeli, mke wa Ezekieli, Nebukadneza.
Wazo Kuu
Hukumu na utukufu wa Mwenyezi Mungu.
Mambo Muhimu
Ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa taifa la Israeli kuhusu hukumu ya dhambi zao, hukumu ya watu wa mataifa, na tumaini kwa Waisraeli katika siku za mwisho.
Yaliyomo
Mwito wa Ezekieli (1:1–3:27)
Hali ya dhambi ya Yerusalemu na maangamizi (4:1–24:27)
Unabii dhidi ya mataifa ya kigeni (25:1–32:32)
Matumaini ya kurejeshwa (33:1–39:29)
Hekalu jipya na ukuhani kufanywa upya (40:1–44:31)
Israeli kurejeshwa nchi yao (45:1–48:35).
Iliyochaguliwa sasa
Ezekieli Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.