Kutoka 40:34-38
Kutoka 40:34-38 NEN
Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa BWANA ukaijaza Maskani ya Mungu. Mose hakuweza kuingia ndani ya Hema la Kukutania kwa sababu wingu lilikuwa limetua juu ya Hema, nao utukufu wa BWANA ukaijaza Maskani ya Mungu. Katika safari yote ya Waisraeli, kila wakati wingu lilipoinuka kutoka juu ya Maskani ya Mungu, wangeondoka; lakini kama wingu halikuinuka, hawakuondoka, mpaka siku lilipoinuka. Kwa hiyo wingu la BWANA lilikuwa juu ya maskani mchana, na moto ulikuwa katika hilo wingu wakati wa usiku, machoni pa nyumba yote ya Israeli siku zote za safari zao.