Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 34:5-9

Kutoka 34:5-9 NEN

Kisha BWANA akashuka katika wingu akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina lake, BWANA. BWANA akapita mbele ya Mose, akitangaza, “BWANA, BWANA, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne.” Mara Mose akasujudu na kuabudu. Mose akasema, “Ee BWANA, kama nimepata kibali mbele zako, basi BWANA uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kutoka 34:5-9