Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 28:40-43

Kutoka 28:40-43 NENO

Watengenezee wana wa Haruni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima. Baada ya kumvika Haruni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, wapake mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. “Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani. Haruni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa. “Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Haruni na vizazi vyake.