Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 24:1-8

Kutoka 24:1-8 NENO

Kisha Mungu akamwambia Musa, “Njooni huku juu kwa BWANA, wewe na Haruni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli. Mniabudu kwa mbali, lakini Musa peke yake ndiye atakayemkaribia BWANA; wengine wasije karibu. Nao watu wasije wakapanda pamoja naye.” Musa alipoenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za BWANA, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema BWANA tutakifanya.” Ndipo Musa akaandika kila kitu BWANA alichokuwa amesema. Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli. Kisha akawatuma vijana wanaume Waisraeli, nao wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu za mafahali wachanga kuwa sadaka za amani kwa BWANA. Musa akachukua nusu ya damu ya wale wanyama na kuiweka kwenye mabakuli, na nusu nyingine akainyunyiza juu ya madhabahu. Kisha akachukua kile Kitabu cha Agano na kuwasomea watu. Nao wakajibu, “Tutafanya kila kitu alichosema BWANA, nasi tutatii.” Ndipo Musa akachukua ile damu, akawanyunyizia wale watu, akasema, “Hii ni damu ya agano ambalo BWANA amelifanya nanyi kufuatana na maneno haya yote.”