Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 13:1-13

Kutoka 13:1-13 NENO

Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Niwekeeni wakfu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume. Kila mtoto wa kwanza aliye kifungua mimba miongoni mwa Waisraeli ni mali yangu, akiwa wa mwanadamu au wa mnyama.” Ndipo Musa akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile chochote kilichotiwa chachu. Leo, katika mwezi wa Abibu, mnatoka. Mwenyezi Mungu atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi inayotiririka maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu: Kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu na katika siku ya saba utamfanyia Mwenyezi Mungu sikukuu. Kwa muda wa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu, pasionekane kitu chochote kilicho na chachu miongoni mwako, wala chachu yoyote isionekane popote ndani ya mipaka yako. Siku ile utamwambia mwanao, ‘Nafanya hivi kwa sababu ya jambo ambalo Mwenyezi Mungu alinitendea nilipotoka katika nchi ya Misri.’ Adhimisho hili, litakuwa kama alama kwenye mkono wako na ukumbusho katika paji lako la uso, kwamba sheria ya Mwenyezi Mungu inapaswa iwe kinywani mwako. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu. Ni lazima ulishike agizo hili kwa wakati uliopangwa mwaka baada ya mwaka. “Baada ya Mwenyezi Mungu kukuingiza katika nchi ya Wakanaani na kukupa nchi hiyo, kama alivyokuahidi kwa kiapo na kwa baba zako, inakupasa kumtolea Mwenyezi Mungu kila mzaliwa wa kwanza. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya Mwenyezi Mungu. Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo, lakini kama hutamkomboa, utamvunja shingo yake. Kila mzaliwa wa kwanza mwanaume miongoni mwa wana wenu utamkomboa.

Video ya Kutoka 13:1-13