Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 12:21-28

Kutoka 12:21-28 NENO

Ndipo Musa akawaita wazee wote wa Israeli na kuwaambia, “Nendeni mara moja mkachague wanyama kwa ajili ya jamaa zenu, mkachinje mwana-kondoo wa Pasaka. Chukueni kitawi cha hisopo, mkichovye kwenye damu iliyopo kwenye sinia, na kuipaka sehemu ya hiyo damu kwenye vizingiti, na kwenye miimo yote miwili ya milango. Mtu yeyote asitoke nje ya mlango wa nyumba yake hadi asubuhi. Mwenyezi Mungu apitapo katika nchi yote kuwapiga Wamisri, ataiona damu juu ya vizingiti na kwenye miimo ya milango, naye atapita juu, wala hatamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zenu na kuwapiga ninyi. “Shikeni maagizo haya yawe kanuni ya kudumu kwenu na kwa ajili ya wazao wenu. Mtakapoingia katika nchi Mwenyezi Mungu atakayowapa kama alivyoahidi, shikeni desturi hii. Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’ Basi waambieni, ‘Hii ni dhabihu ya Pasaka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye alipita juu ya nyumba za Waisraeli katika nchi ya Misri, na hakudhuru nyumba zetu alipowapiga Wamisri.’ ” Ndipo Waisraeli walisujudu na kuabudu. Waisraeli wakafanya kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa na Haruni.

Video ya Kutoka 12:21-28