Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waefeso 5:8-20

Waefeso 5:8-20 NEN

Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru (kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli), nanyi tafuteni yale yanayompendeza Bwana. Msishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni. Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini. Lakini kila kitu kilichowekwa nuruni, huonekana, kwa kuwa nuru ndiyo hufanya kila kitu kionekane. Hii ndiyo sababu imesemekana: “Amka, wewe uliyelala, ufufuke kutoka kwa wafu, naye Kristo atakuangazia.” Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini mapenzi ya Bwana. Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho. Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu, siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Waefeso 5:8-20