Kumbukumbu 6:4-7
Kumbukumbu 6:4-7 NEN
Sikia, ee Israeli: BWANA Mungu wako, BWANA ni mmoja. Mpende BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.