Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 4:1-7

Kumbukumbu 4:1-7 NEN

Sikia sasa, ee Israeli, amri na sheria nitakazokufundisha wewe. Zifuate ili upate kuishi na uingie kuimiliki nchi ambayo BWANA, Mungu wa baba zako anawapa. Usiongeze wala usipunguze chochote ninachowaamuru ninyi, ila myashike maagizo ya BWANA Mungu wenu ambayo nawapa. Mliona kwa macho yenu wenyewe kile BWANA alichokifanya kule Baal-Peori. BWANA Mungu wenu aliwaangamiza kutoka miongoni mwenu kila mmoja aliyemfuata Baali wa Peori, lakini ninyi nyote mlioshikamana na BWANA kwa uthabiti, Mungu wenu, mko hai mpaka leo. Tazama, nimewafundisha amri na sheria kama BWANA Mungu wangu alivyoniamuru mimi, ili mzifuate katika nchi mnayoiingia kuimiliki. Zishikeni kwa uangalifu, kwa kuwa hii itaonyesha hekima na ufahamu wenu kwa mataifa, ambayo yatasikia kuhusu amri zote hizi, nao watasema, “Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na ufahamu.” Ni taifa gani jingine lililo kubwa kiasi cha kuwa na miungu yao iliyo karibu nao kama BWANA Mungu wetu alivyo karibu nasi wakati wowote tunapomwomba?

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kumbukumbu 4:1-7

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha