Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 31:9-13

Kumbukumbu 31:9-13 NENO

Kwa hiyo Musa akaandika sheria hii na kuwapa makuhani, wana wa Lawi, waliochukua Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu na wazee wote wa Israeli. Kisha Musa akawaamuru, akasema: “Mwishoni mwa kila miaka saba, katika mwaka wa kufuta madeni, wakati wa Sikukuu ya Vibanda, Waisraeli wote wanapokuja mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, mahali atakapopachagua, utasoma sheria hii mbele yao masikioni mwao. Kusanya watu wote, wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili waweze kusikia na kujifunza kumcha Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kuzingatia maneno yote ya sheria hii. Watoto wao, ambao hawaijui sheria hii, lazima waisikie na kujifunza kumcha Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa muda mtakaoishi katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki.”