Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 28:1-14

Kumbukumbu 28:1-14 NEN

Kama ukimtii BWANA Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, BWANA Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia. Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtii BWANA Mungu wako: Utabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ngʼombe, na wana-kondoo wa makundi yako. Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa. Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo. BWANA atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. BWANA ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako. BWANA Mungu wako atakubariki katika nchi anayokupa. BWANA atakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, kama ukishika maagizo ya BWANA Mungu wako na kwenda katika njia zake. Kisha mataifa yote ya dunia wataona kuwa unaitwa kwa jina la BWANA, nao watakuogopa. BWANA atakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa tumbo lako, katika wanyama wachanga wa mifugo yako na katika mazao ya ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwapa. BWANA atafungua mbingu, ghala zake za baraka, kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mikono yako. Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa yeyote. BWANA atakufanya kichwa, wala si mkia. Kama utazingatia maagizo ya BWANA Mungu wako ninayokupa siku hii ya leo na kuyafuata kwa bidii, daima utakuwa juu, kamwe hutakuwa chini. Usihalifu amri zangu zozote ninazokupa leo, kwa kwenda kuume au kushoto, kwa kufuata miungu mingine na kuitumikia.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kumbukumbu 28:1-14

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha