Kumbukumbu 1:6-8
Kumbukumbu 1:6-8 NENO
Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, alisema nasi huko Horebu, “Mmekaa muda wa kutosha katika mlima huu. Vunjeni kambi, msonge mbele kuelekea nchi ya vilima ya Waamori; nendeni kwa watu wote ambao ni majirani wa Araba, katika milima, Shefela, katika Negebu na kandokando ya pwani, hadi nchi ya Wakanaani na hadi Lebanoni, na kufika mto mkubwa Frati. Tazama, nimewapa ninyi nchi hii. Ingieni mkaimiliki nchi ambayo Mwenyezi Mungu aliapa kuwa angewapa baba zenu, Ibrahimu, Isaka na Yakobo, pamoja na uzao wao baada yao.”