Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Danieli Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kinatoa kumbukumbu za Danieli wakati wa utumishi wake wa muda mrefu katika falme za Babeli na Uajemi. Alipokuwa mateka katika jumba la mfalme huko Babeli, Danieli alipandishwa cheo na kupewa wadhifa wa juu baada ya kumwambia Nebukadneza ndoto yake na fasiri yake. Katika mwongo wa mwisho wa maisha yake, Danieli alipata funuo kadha wa kadha kutoka kwa Mwenyezi Mungu zilizowiana na ndoto ya Nebukadneza. Ndoto hizo zilionesha kuinuka na kuanguka kwa falme za dunia zilizostawi, ambazo hatimaye falme hizi zinafikia ukomo na Mwenyezi Mungu anainua ufalme wa milele. Danieli, kama Myahudi mcha Mwenyezi Mungu aliyekuwa mwombaji na msomaji wa Maandiko, alikuwa anawajali sana watu wake wa Israeli. Alihakikishiwa na Mwenyezi Mungu kwamba wangefanywa imara tena.
Mwandishi
Danieli.
Kusudi
Kueleza na kuonesha uweza wa Mwenyezi Mungu kwamba ndiye anayetawala mbingu na nchi na kwamba falme zote za wanadamu ziko chini yake. Pia, kuonesha jinsi Mwenyezi Mungu anavyoweza kuokoa wale wanaomtumaini.
Mahali
Babeli.
Tarehe
Mnamo 536–530 K.K.
Wahusika Wakuu
Danieli, Shadraki, Meshaki, Abednego, Nebukadneza, Belshaza na Dario.
Wazo Kuu
Ukuu wa Mwenyezi Mungu ambaye anatawala historia yote.
Mambo Muhimu
Maono ya Danieli yanaonesha mpango wa Mwenyezi Mungu kwa vizazi vyote, pamoja na kutabiri kuhusu ujio wa Masihi.
Yaliyomo
Danieli na rafiki zake wahudumu chini ya wafalme wa Babeli (1:1–5:31)
Danieli katika tundu la simba (6:1–6:28)
Maono wakati wa utawala wa Belshaza (7:1–8:27)
Ndoto ya Danieli na majuma sabini (9:1-27)
Maono ya mwisho ya Danieli (10:1–12:13).

Iliyochaguliwa sasa

Danieli Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia