Wakolosai 3:18-21
Wakolosai 3:18-21 NENO
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana Isa. Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe wakali kwao. Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hii inampendeza Bwana Isa. Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.