Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 14:21-28

Matendo 14:21-28 NEN

Wakahubiri habari njema katika mji huo na kupata wanafunzi wengi. Kisha wakarudi Listra, Ikonio na Antiokia, wakiwaimarisha wanafunzi na kuwatia moyo waendelee kudumu katika imani. Wakawaonya wakisema, “Imetupasa kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kupitia katika taabu nyingi.” Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kanisa, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana waliyemwamini. Kisha wakapitia Pisidia wakafika Pamfilia. Baada ya kuhubiri neno la Mungu huko Perga, wakateremkia Atalia. Kutoka Atalia wakasafiri baharini wakarudi Antiokia, ambako walikuwa wamesifiwa kwa ajili ya neema ya Mungu kutokana na ile huduma waliyokuwa wameikamilisha. Walipowasili Antiokia wakaliita kanisa pamoja na kutoa taarifa ya yale yote Mungu aliyokuwa ametenda kupitia kwao na jinsi alivyokuwa amefungua mlango wa imani kwa ajili ya watu wa Mataifa. Nao wakakaa huko pamoja na wanafunzi kwa muda mrefu.

Video for Matendo 14:21-28

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Matendo 14:21-28