Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

3 Yohana Utangulizi

Utangulizi
Waraka wa tatu wa Yohana uliandikiwa Gayo, ambaye alikuwa kiongozi muhimu katika fulani. Alielekezwa kuwasaidia na kuwahudumia wajumbe wa Mwenyezi Mungu waliotembelea kundi la waumini. Pia alipewa onyo kuhusu Deotrefe, kwa tabia yake ya kukosa ushirikiano. Yohana alieleza tarajio lake la kuja na kushughulikia tatizo hili mwenyewe.
Mwandishi
Mtume Yohana.
Kusudi
Yohana anamwandikia Gayo akimpa onyo kuhusu Deotrefe, kwa tabia yake ya kukosa ushirikiano.
Mahali
Efeso.
Tarehe
Mnamo 90 B.K.
Wahusika Wakuu
Yohana, Gayo, Deotrefe, na Demetrio.
Wazo Kuu
Wajibu binafsi wa Gayo kuhusu watumishi wa kweli na wa uongo.
Mambo Muhimu
Yohana anamtakia Gayo kufanikiwa katika mambo yote, na pia anamwagiza asiige lililo baya bali aige lililo jema.
Yaliyomo
Salamu (1-4)
Gayo anatiwa moyo (5-8)
Deotrefe anakemewa (9-10)
Demetrio anasifiwa (11-12)
Hitimisho (13-15).

Iliyochaguliwa sasa

3 Yohana Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia