Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

3 Yohana 1:11-14

3 Yohana 1:11-14 NEN

Rafiki mpendwa, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Yeyote atendaye mema atoka kwa Mungu, bali atendaye mabaya hajamwona Mungu. Kila mtu ameshuhudia mema kuhusu Demetrio, vivyo hivyo hata na hiyo kweli yenyewe. Sisi pia twashuhudia mema juu yake, nanyi mwajua kwamba ushuhuda wetu ni kweli. Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kuandika kwa kalamu na wino. Badala yake, nataraji kukuona upesi, nasi tutaongea pamoja ana kwa ana.