Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Timotheo 1:12-18

2 Timotheo 1:12-18 NEN

Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile. Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu. Ilinde ile amana uliyokabidhiwa kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu. Unajua ya kuwa watu wote katika Asia wameniacha, miongoni mwao wamo Filego na Hermogene. Bwana akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara wala hakuionea aibu minyororo yangu. Badala yake, alipokuwa Rumi, alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata. Bwana na amjalie kupata rehema zake siku ile! Nawe unajua vyema jinsi alivyonisaidia huko Efeso.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Timotheo 1:12-18

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha