Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samweli Utangulizi

Utangulizi
Kitabu cha 2 Samweli kinaendeleza historia ya kuanzishwa kwa ufalme katika Israeli. Kinaanza na kifo cha Sauli, na kuendelea na habari za kutawazwa kwa Daudi kukalia kiti cha ufalme cha Israeli, na pia kipindi chote cha utawala wake. Kinaweka kumbukumbu ya vita na matukio mengine ya wakati wa utawala wa Daudi kama vile kutekwa kwa mji wa Yerusalemu (5:6-16), dhambi ya Daudi na Bathsheba (11:1-27), na uasi wa Absalomu (13:1-20).
Mwandishi
Haijulikani kwa uhakika. Wengine wamesema inawezekana ikawa ni Zabudi, mwanawe Nathani; pia kitabu kina habari zilizoandikwa na Nathani na Gadi.
Kusudi
Kitabu hiki kinamwonyesha Daudi kama mtu muhimu ambaye chini ya uongozi wake taifa la Israeli lilifikia kilele cha umoja na nguvu kuliko nyakati nyingine zote katika historia lake.
Mahali
Katika nchi ya Israeli chini ya utawala wa Mfalme Daudi.
Tarehe
Kitabu hiki kinadhaniwa kiliandikwa mwaka wa 930 K.K.
Wahusika Wakuu
Daudi, Yoabu, Bathsheba, Nathani na Absalomu.
Wazo Kuu
Kitabu hiki kinashughulika zaidi na miaka arobaini ya utawala wa Mfalme Daudi, kikionyesha jinsi ambavyo ustawi wa watu wote kifamilia na kitaifa umefungwa katika hali ya kiroho na ya kimaadili ya kiongozi wao. Uadilifu au upotovu wa kiongozi huamua ustawi au kudidimia kwa jamii au taifa.
Mambo Muhimu
Kukua kwa ufalme wa Israeli na utawala wa Mfalme Daudi.
Mgawanyo
Daudi mfalme wa Yuda (1:1–4:12)
Daudi anaiunganisha Israeli (5:1–24:25).

Iliyochaguliwa sasa

2 Samweli Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha