Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samweli 19:40-43

2 Samweli 19:40-43 NENO

Mfalme alipovuka kwenda Gilgali, Kimhamu akavuka pamoja naye. Vikosi vyote vya Yuda na nusu ya vikosi vya Israeli vilimvusha mfalme. Baada ya kitambo kidogo, wanaume wote wa Israeli wakaja kwa mfalme na kumwambia, “Kwa nini ndugu zetu, wanaume wa Yuda, wamemrudisha mfalme kwa siri bila kutushirikisha, na kumvusha ng’ambo ya Yordani, yeye na nyumba yake, pamoja na watu wake wote?” Wanaume wote wa Yuda wakawajibu wanaume wa Israeli, “Tulifanya hivi kwa sababu mfalme ni jamaa yetu wa karibu. Kwa nini mnakasirikia jambo hili? Je, tumekula kitu chochote cha mfalme? Je, tumejichukulia kitu chochote kwa ajili yetu wenyewe?” Ndipo wanaume wa Israeli wakawajibu wanaume wa Yuda, “Tunayo haki mara kumi kwa mfalme; sisi tunahusika zaidi na Daudi kuliko ninyi. Kwa nini basi mnatudharau? Je, hatukuwa wa kwanza kuzungumza kuhusu kumrudisha mfalme nyumbani?” Lakini wanaume wa Yuda wakajibu kwa ukali hata kuliko wanaume wa Israeli.