Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samweli 12:9-14

2 Samweli 12:9-14 NEN

Kwa nini ulilidharau neno la BWANA kwa kufanya lililo ovu machoni pake? Ulimuua Uria, Mhiti kwa upanga na kumchukua mke wake awe mkeo. Ulimuua kwa upanga wa Waamoni. Basi kwa hiyo, upanga hautaondoka nyumbani mwako kamwe kwa sababu ulinidharau mimi na kumchukua mke wa Uria, Mhiti kuwa mkeo.’ “Hili ndilo asemalo BWANA: ‘Kutoka kwa nyumba yako mwenyewe nitaleta maafa juu yako. Mbele ya macho yako mwenyewe nitatwaa wake zako na kumpa yeye aliye wa karibu nawe, naye atakutana kimwili na wake zako mchana mwangavu. Ulifanya kwa siri, lakini nitalifanya jambo hili wakati wa mchana mwangavu mbele ya Israeli yote.’ ” Ndipo Daudi akamjibu Nathani, “Nimefanya dhambi dhidi ya BWANA.” Nathani akamjibu, “BWANA amekuondolea dhambi yako. Hutakufa. Lakini kwa sababu kwa kufanya hili umefanya adui za BWANA kuonyesha dharau kabisa, mwana atakayezaliwa kwako atakufa.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Samweli 12:9-14