Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Petro 1:5-9

2 Petro 1:5-9 NEN

Kwa sababu hii hasa, jitahidini sana katika imani yenu kuongeza wema; na katika wema, maarifa; katika maarifa, kiasi; katika kiasi, saburi; katika saburi, utauwa; katika utauwa, upendano wa ndugu; na katika upendano wa ndugu, upendo. Kwa maana haya yakiwa ndani yenu kwa wingi na kuzidi kuongezeka, yanawasaidia msikose bidii wala kutozaa matunda katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. Lakini mtu yeyote asipokuwa na mambo haya haoni mbali, na ni kipofu, naye amesahau kule kutakaswa kutoka dhambi zake za zamani.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Petro 1:5-9