Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wakorintho 13:10-14

2 Wakorintho 13:10-14 NEN

Hii ndiyo sababu nawaandikia mambo haya wakati sipo, ili nikija nisiwe mkali katika kutumia mamlaka yangu, mamlaka Bwana aliyonipa ya kuwajenga ninyi wala si ya kuwabomoa. Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, mkafarijike, kuweni wa nia moja, kaeni kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu. Watakatifu wote wanawasalimu. Neema ya Bwana Yesu Kristo, na upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Amen.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Wakorintho 13:10-14