2 Nyakati Utangulizi
Utangulizi
Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati kinaendelea kuzungumzia historia ya Yuda. Sura 1–9 zinaelezea kujengwa kwa Hekalu wakati wa utawala wa Mfalme Solomoni. Sura 10–36 zinaelezea historia ya Ufalme wa Yuda mpaka kufikia kuharibiwa kwa Yerusalemu na watu kupelekwa uhamishoni Babeli. Kitabu hiki kinazungumzia jinsi uhusiano wa watu na Mungu ni jambo la muhimu kuliko vitu vyote. Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati kinaambatana na vitabu vya 1 na 2 Wafalme kikitoa ufafanuzi wake. Ufalme wa Kaskazini, yaani Israeli, haujatajwa kabisa katika historia ya kitabu hiki.
Mwandishi
Mapokeo ya Kiyahudi husema ni Ezra.
Kusudi
Kusudi la kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati ni kuliunganisha taifa katika ibada ya Mungu wa kweli kwa kuonyesha viwango vyake katika kuwahukumu wafalme. Habari za wafalme wenye haki wa Yuda na wapinzani wao wa kidini nyakati zao za utawala zimewekwa wazi, na dhambi za wafalme waovu zimewekwa wazi pia.
Mahali
Yerusalemu, na katika Hekalu.
Tarehe
Kama mwaka wa 430 K.K.
Wahusika Wakuu
Solomoni, Malkia wa Sheba, Rehoboamu, Asa, Yehoshafati, Yehoramu, Yoashi, Uzia, Ahazi, Hezekia, Manase na Yosia.
Wazo Kuu
Kitabu hiki kinaonyesha mpango wa Mungu kwa Israeli. Pia kinaonyesha kwa nini ufalme wa Daudi haukuruhusiwa kuendelea kwa muda mrefu. Kitabu hiki, kama kile cha kwanza, kinaonyesha wajibu wa Mungu katika historia ya watu wake na mwingiliano kati ya maisha ya kiroho na ya kisiasa. Wafalme wanapimwa kwa jinsi walivyokuwa waaminifu kwa Mungu.
Mambo Muhimu
Utawala wa Solomoni, kujengwa kwa Hekalu, kuasi kwa makabila kumi, habari za wafalme wa Yuda, na kuharibiwa kwa ufalme wa Yuda na Wababeli mwaka wa 586 K.K.
Mgawanyo
Utawala wa Solomoni (1:1–9:31)
Wafalme wa Yuda (10:1–36:14)
Kuharibiwa kwa Yerusalemu (36:15-23).
Iliyochaguliwa sasa
2 Nyakati Utangulizi: NEN
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.
Used with Permission. All Rights Reserved Worldwide.