Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nyakati 27

27
Yothamu mfalme wa Yuda
(2 Wafalme 15:32-38)
1Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki. 2Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa Mwenyezi Mungu. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya. 3Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Mwenyezi Mungu na kufanya kazi kubwa kwenye ukuta katika kilima cha Ofeli. 4Akajenga miji katika nchi ya vilima ya Yuda, pamoja na ngome na minara mwituni.
5Yothamu akafanya vita na mfalme wa Waamoni na kumshinda. Mwaka ule Waamoni wakamlipa talanta mia moja#27:5 Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75. za fedha, kori elfu kumi#27:5 Kori 10,000 za ngano ni sawa na tani 2.2. za ngano, na kori elfu kumi za shayiri. Waamoni wakamletea kiasi hicho hicho mwaka wa pili na wa tatu.
6Yothamu akaendelea kuwa na nguvu kwa sababu alienenda kwa ukamilifu mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wake.
7Matukio mengine ya utawala wa Yothamu, pamoja na vita vyake vyote na vitu vingine alivyofanya, vimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. 8Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. 9Yothamu akalala na baba zake na akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Ahazi mwanawe akawa mfalme baada yake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nyakati 27: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia