Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wathesalonike 5:15-28

1 Wathesalonike 5:15-28 NEN

Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote. Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu. Msiuzime moto wa Roho Mtakatifu; msiyadharau maneno ya unabii. Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema. Jiepusheni na uovu wa kila namna. Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo. Ndugu, tuombeeni. Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu. Nawaagizeni mbele za Bwana mhakikishe kuwa ndugu wote wanasomewa barua hii. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi. Amen.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Wathesalonike 5:15-28