Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Samweli 7:2-6

1 Samweli 7:2-6 NEN

Sanduku la BWANA lilibakia huko Kiriath-Yearimu kwa muda mrefu, yaani jumla ya miaka ishirini, nao watu wa Israeli wakaomboleza na kumtafuta BWANA. Naye Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, “Ikiwa mtamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi iacheni miungu migeni na Maashtorethi na kujitoa wenyewe kwa BWANA na kumtumikia yeye peke yake, naye atawaokoa ninyi na mkono wa Wafilisti.” Hivyo Waisraeli wakaweka mbali Mabaali yao na Maashtorethi, nao wakamtumikia BWANA peke yake. Kisha Samweli akasema, “Wakusanyeni Israeli wote huko Mispa, nami nitawaombea ninyi kwa BWANA.” Walipokwisha kukutanika huko Mispa, walichota maji na kuyamimina mbele za BWANA. Siku hiyo walifunga na wakaungama, wakisema, “Tumetenda dhambi dhidi ya BWANA.” Naye Samweli alikuwa kiongozi wa Israeli huko Mispa.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha