Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Samweli 16:10-12

1 Samweli 16:10-12 NEN

Yese alikuwa na wana saba aliowapitisha mbele ya Samweli, lakini Samweli akamwambia, “BWANA hajawachagua hawa.” Hivyo akamuuliza Yese, “Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?” Yese akajibu, “Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo.” Samweli akasema, “Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike.” Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza. Ndipo BWANA akasema, “Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Samweli 16:10-12