1 Wafalme 9:24-28
1 Wafalme 9:24-28 NENO
Baada ya binti Farao kuja kutoka Mji wa Daudi na kuingia jumba la kifalme ambalo Sulemani alikuwa amemjengea, Sulemani akajenga Milo. Sulemani akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani mara tatu kwa mwaka juu ya madhabahu aliyokuwa amemjengea Mwenyezi Mungu. Pamoja na hizo dhabihu, akafukiza uvumba mbele za Mwenyezi Mungu, hivyo kutimiza kanuni za Hekalu. Mfalme Sulemani pia akatengeneza meli huko Esion-Geberi, iliyo karibu na Elathi katika Edomu, kwenye ukingo wa Bahari ya Shamu. Naye Hiramu akawatuma watu wake; mabaharia walioijua bahari, kuhudumu katika hizo meli pamoja na watu wa Sulemani. Wakasafiri kwa bahari hadi Ofiri na kurudi na talanta mia nne na ishirini (420) za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Sulemani.