1 Wafalme 19:11-13
1 Wafalme 19:11-13 NEN
BWANA akasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za BWANA, kwa kuwa BWANA yu karibu kupita hapo.” Kisha upepo mwingi na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za BWANA, lakini BWANA hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la nchi, lakini BWANA hakuwamo kwenye lile tetemeko. Baada ya tetemeko la nchi ukaja moto, lakini BWANA hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunongʼona. Eliya alipoisikia, akafunika uso kwa vazi lake, akatoka na kusimama kwenye mdomo wa pango. Kisha ile sauti ikamwambia, “Eliya, unafanya nini hapa?”