Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Yohana 5:13-17

1 Yohana 5:13-17 NEN

Nawaandikia mambo haya ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu ili mpate kujua ya kuwa mnao uzima wa milele. Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Nasi kama tunajua atusikia, lolote tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba. Kama mtu akimwona ndugu yake akitenda dhambi isiyo ya mauti, inampasa aombe, naye Mungu atampa uzima mtu huyo. Ninamaanisha wale ambao dhambi yao si ya mauti. Iko dhambi ya mauti, sisemi kwamba utaomba kwa ajili ya hiyo. Jambo lolote lisilo la haki ni dhambi, lakini iko dhambi isiyo ya mauti.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Yohana 5:13-17