Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Yohana 5:1-12

1 Yohana 5:1-12 NENO

Kila mtu anayeamini kwamba Isa ndiye Al-Masihi amezaliwa na Mungu, na yeyote ampendaye Baba humpenda pia mtoto aliyezaliwa naye. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu, kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri zake. Huku ndiko kumpenda Mungu, yaani kuzitii amri zake. Nazo amri zake si nzito. Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani hiyo imani yetu. Ni nani yule aushindaye ulimwengu? Ni yule tu aaminiye kwamba Isa ni Mwana wa Mungu. Huyu ndiye alikuja kwa maji na damu, yaani Isa Al-Masihi. Hakuja kwa maji peke yake, bali kwa maji na damu. Naye Roho wa Mungu ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni: hao ni Baba, Neno na Roho wa Mungu. Hawa watatu ni umoja. Pia wako mashahidi watatu duniani]: hao ni Roho, Maji na Damu; hawa watatu wanakubaliana katika umoja. Kama tunaukubali ushuhuda wa wanadamu, basi ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi, kwa kuwa huu ndio ushuhuda wa Mungu kwamba amemshuhudia Mwanawe. Kila mtu amwaminiye Mwana wa Mungu anao huu ushuhuda moyoni mwake. Kila mtu asiyemwamini Mungu amemfanya yeye kuwa mwongo, kwa sababu hakuamini ushuhuda Mungu alioutoa kuhusu Mwanawe. Huu ndio ushuhuda: kwamba Mungu ametupatia uzima wa milele, nao huo uzima umo katika Mwanawe. Aliye naye Mwana wa Mungu anao uzima, yeye asiye na Mwana wa Mungu hana uzima.