1 Yohana 4:9-11
1 Yohana 4:9-11 NENO
Hivi ndivyo Mungu alivyoonesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake. Hili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu. Wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana.