Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Yohana 3:21-24

1 Yohana 3:21-24 NENO

Wapendwa, kama mioyo yetu haituhukumu, tunao ujasiri mbele za Mungu, lolote tuombalo, twalipokea kutoka kwake, kwa sababu tumezitii amri zake na kutenda yale yanayompendeza. Hii ndiyo amri yake: kwamba tuliamini Jina la Mwanawe, Isa Al-Masihi, na kupendana sisi kwa sisi kama yeye alivyotuamuru. Wale wote wanaozishika amri zake hukaa ndani yake na yeye ndani yao. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba anakaa ndani yetu. Nasi twajua hili kupitia kwa Roho wa Mungu, yule aliyetupatia.