1 Wakorintho 15:57-58
1 Wakorintho 15:57-58 NENO
Lakini Mungu apewe shukrani, yeye atupaye ushindi kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa hiyo, ndugu zangu wapendwa, simameni imara. Msitikisike. Mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana si bure.