Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wakorintho 14:26-33

1 Wakorintho 14:26-33 NENO

Basi tuseme nini ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana wimbo, au neno la mafundisho, au ufunuo, lugha mpya au atatafsiri. Mambo yote yatendeke kwa ajili ya kulijenga kundi la waumini. Kama mtu yeyote akinena kwa lugha, basi waseme watu wawili au watatu, si zaidi, mmoja baada ya mwingine, na lazima awepo mtu wa kutafsiri. Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, hao watu na wanyamaze kimya katika kundi la waumini, na wanene na nafsi zao wenyewe na Mungu. Manabii wawili au watatu wanene, na wengine wapime kwa makini yale yasemwayo. Kama mtu yeyote aliyeketi karibu, akipata ufunuo, basi yule wa kwanza na anyamaze. Kwa maana wote mnaweza kutoa unabii, mmoja baada ya mwingine, ili kila mtu apate kufundishwa na kutiwa moyo. Roho za manabii huwatii manabii. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa amani. Kama ilivyo katika makusanyiko yote ya watakatifu