1 Wakorintho 10:6-13
1 Wakorintho 10:6-13 NENO
Basi mambo haya yalifanyika kama mifano ili kutuzuia tusiweke mioyo yetu katika mambo maovu kama wao walivyofanya. Msiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyokuwa, kama ilivyoandikwa, “Watu waliketi chini kula na kunywa, kisha wakainuka kucheza na kufanya sherehe za kipagani.” Wala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu elfu ishirini na tatu kwa siku moja. Wala tusimjaribu Al-Masihi, kama baadhi yao walivyofanya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. Msinung’unike kama baadhi yao walivyofanya, wakaangamizwa na malaika mharibifu. Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wengine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia. Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kushinda ili mweze kustahimili.