Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wakorintho 10:6-13

1 Wakorintho 10:6-13 SRUV

Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu elfu ishirini na tatu. Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka. Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakauawa na mharibifu. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiwa na miisho ya nyakati. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili.