Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati 2

2
Wana wa Israeli
1Hawa walikuwa wana wa Israeli: Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni, 2Dani, Yusufu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.
Yuda
Hadi wana wa Hesroni
3Wana wa Yuda walikuwa:
Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti Shua.
(Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Mwenyezi Mungu, kwa hiyo Mwenyezi Mungu alimuua.)
4Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera.
Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.
5Wana wa Peresi walikuwa:
Hesroni na Hamuli.
6Wana wa Zera walikuwa:
Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Darda. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.
7Mwana wa Karmi alikuwa:
Akari#2:7 maana yake Taabisha; pia anaitwa Akani (Yoshua 6:1-26; 22:20), ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutochukua vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa.
8Mwana wa Ethani alikuwa:
Azariya.
9Wana wa Hesroni walikuwa:
Yerameeli, Ramu na Kalebu.
Kuanzia Ramu mwana wa Hesroni
10Ramu alimzaa Aminadabu,
naye Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda.
11Nashoni akamzaa Salmoni,
Salmoni akamzaa Boazi,
12Boazi akamzaa Obedi,
Obedi akamzaa Yese.
13Yese akawazaa
Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu,
wa tatu Shimea, 14wa nne Nethaneli,
wa tano Radai, 15wa sita Osemu,
na wa saba Daudi.
16Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili.
Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli.
17Abigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri Mwishmaeli.
Kalebu mwana wa Hesroni
18Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu:
Yesheri, Shobabu na Ardoni.
19Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrata, aliyemzalia Huri.
20Huri akamzaa Uri, naye Uri akamzaa Bezaleli.
21Hatimaye, Hesroni alipokuwa na umri wa miaka sitini, alimwoa binti Makiri, babaye Gileadi. Akakutana kimwili naye, akamzalia Segubu.
22Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na tatu katika Gileadi.
23(Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na makazi yake; jumla ilikuwa miji sitini.)
Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.
24Baada ya Hesroni kufa huko Kalebu-Efrata, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.
Yerameeli mwana wa Hesroni
25Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa:
Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya. 26Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu.
27Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa:
Maasi, Yamini na Ekeri.
28Wana wa Onamu walikuwa:
Shamai na Yada.
Wana wa Shamai walikuwa:
Nadabu na Abishuri. 29Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, aliyemzalia Abani na Molidi.
30Wana wa Nadabu walikuwa
Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto.
31Apaimu akamzaa:
Ishi aliyekuwa baba wa Sheshani.
Sheshani akamzaa Alai.
32Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa:
Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto.
33Wana wa Yonathani walikuwa:
Pelethi na Zaza.
Hao walikuwa wazao wa Yerameeli.
34Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila watoto wa kike tu.
Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha. 35Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai.
36Atai akamzaa Nathani,
Nathani akamzaa Zabadi,
37Zabadi akamzaa Eflali,
Eflali akamzaa Obedi,
38Obedi akamzaa Yehu,
Yehu akamzaa Azaria,
39Azaria akamzaa Helesi,
Helesi akamzaa Eleasa,
40Eleasa akamzaa Sismai,
Sismai akamzaa Shalumu,
41Shalumu akamzaa Yekamia,
naye Yekamia akamzaa Elishama.
Koo za Kalebu
42Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa:
Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu,
naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.
43Hebroni alikuwa na wana wanne:
Kora, Tapua, Rekemu na Shema.
44Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu
na Rekemu alikuwa baba wa Shamai.
45Shamai akamzaa Maoni,
naye Maoni akamzaa Beth-Suri.
46Efa, suria wa Kalebu aliwazaa:
Harani, Mosa na Gazezi.
Harani alikuwa baba wa Gazezi.
47Wana wa Yadai walikuwa:
Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.
48Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye
Sheberi na Tirhana.
49Pia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana,
na Sheva babaye Makbena na Gibea.
Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa.
50Hao walikuwa wazao wa Kalebu.
Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, walikuwa:
Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu, 51Salma akamzaa Bethlehemu, naye Harefu akamzaa Beth-Gaderi.
52Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa:
Haroe, nusu ya Wamenuhothi, 53pamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli.
54Wazao wa Salma walikuwa:
Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, nusu ya Wamanahathi, Wazori, 55pamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nyakati 2: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia