Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati 2

2
Wana Wa Israeli
1 Hawa ndio waliokuwa wana wa Israeli:
Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni, 2Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.
Yuda
Hadi Wana Wa Hesroni
3 Wana wa Yuda walikuwa:
Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana alimuua. 4 Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.
5 Wana wa Peresi walikuwa:
Hesroni na Hamuli.
6 Wana wa Zera walikuwa:
Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.
7 Mwana wa Karmi alikuwa:
Akari,#2:7 Akari maana yake Taabisha; pia anaitwa Akani (Yos 6:1-26; 22:20). ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu.
8Mwana wa Ethani alikuwa:
Azariya.
9 Wana wa Hesroni walikuwa:
Yerameeli, Ramu na Kalebu.
Kuanzia Ramu Mwana Wa Hesroni
10 Ramu alimzaa
Aminadabu, na Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda. 11Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi, 12 Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.
13 Yese akawazaa
Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,#2:13 Au: Shima, maana yake Sifa njema (pia 1Sam 16:9; 17:13). 14wa nne Nethaneli, wa tano Radai, 15wa sita Osemu, na wa saba Daudi. 16 Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli. 17 Abigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.
Kalebu Mwana Wa Hesroni
18Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu: Yesheri, Shobabu na Ardoni. 19 Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrathi, ambaye alimzalia Huri. 20 Huri akamzaa Uri, Uri akamzaa Bezaleli.
21 Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu. 22Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na mitatu katika Gileadi. 23 (Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.
24 Baada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.
Yerameeli Mwana Wa Hesroni
25Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa:
Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya. 26Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu.
27Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa:
Maasi, Yamini na Ekeri.
28Wana wa Onamu walikuwa:
Shamai na Yada.
Wana wa Shamai walikuwa:
Nadabu na Abishuri.
29Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, ambaye alimzalia Abani na Molidi.
30Wana wa Nadabu walikuwa
Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto.
31Apaimu akamzaa:
Ishi ambaye alikuwa baba wa Sheshani.
Sheshani akamzaa Alai.
32Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa:
Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto.
33Wana wa Yonathani walikuwa:
Pelethi na Zaza.
Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yerameeli.
34Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila wasichana tu.
Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha. 35Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai.
36 Atai akamzaa Nathani,
Nathani akamzaa Zabadi,
37Zabadi akamzaa Eflali,
Eflali akamzaa Obedi,
38Obedi akamzaa Yehu,
Yehu akamzaa Azaria,
39Azaria akamzaa Helesi,
Helesi akamzaa Eleasa,
40Eleasa akamzaa Sismai,
Sismai akamzaa Shalumu,
41Shalumu akamzaa Yekamia,
naye Yekamia akamzaa Elishama.
Koo Za Kalebu
42Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa:
Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu, naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.
43Hebroni alikuwa na wana wanne:
Kora, Tapua, Rekemu na Shema. 44Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu na Rekemu alikuwa baba wa Shamai. 45 Shamai akamzaa Maoni na Maoni akamzaa Beth-Suri.
46Efa, suria wa Kalebu alikuwa mamaye Harani, Mosa na Gazezi. Harani alikuwa baba wa Gazezi.
47Wana wa Yadai walikuwa:
Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.
48Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye Sheberi na Tirhana. 49 Pia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana, na Sheva babaye Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa. 50 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Kalebu.
Wana wa Huri, mzaliwa mkuu wao wa Efrathi, walikuwa:
Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu, 51Salma akamzaa Bethlehemu, naye Harefu akamzaa Beth-Gaderi.
52Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa:
Haroe, nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi, 53 pamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli.
54 Wazao wa Salma walikuwa:
Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, nusu ya Wamanahathi, Wasori, 55 pamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nyakati 2: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha