1 Nyakati 12:39-40
1 Nyakati 12:39-40 NENO
Watu hawa wakakaa huko na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa sababu jamaa zao zilikuwa zimewapatia mahitaji yao. Pia, majirani zao hata wale walio mbali hadi Isakari, Zabuloni na Naftali, walikuja wakiwaletea vyakula walivyovibeba kwa punda, ngamia, nyumbu na maksai. Kulikuwa na wingi wa unga, maandazi ya tini, maandazi ya zabibu kavu, divai, mafuta, ng’ombe na kondoo, kwa maana kulikuwa na furaha katika Israeli.