Mbona hamniogopi? Nauliza mimi Mwenyezi-Mungu!
Kwa nini hamtetemeki mbele yangu?
Mimi niliweka mchanga uwe mpaka wa bahari,
kizuizi cha daima ambacho bahari haiwezi kuvuka.
Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita;
ingawa yananguruma, hayawezi kuuruka.