1
1 Samueli 15:22
Biblia Habari Njema
Ndipo Samueli akamwambia, “Je, Mwenyezi-Mungu anapendelea zaidi dhabihu za kuteketezwa na matambiko, kuliko kuitii sauti yake? Tazama, kumtii yeye ni bora kuliko matambiko na kumsikiliza kuliko kumtambikia mafuta ya beberu.
Linganisha
Chunguza 1 Samueli 15:22
2
1 Samueli 15:23
Uasi ni sawa na dhambi ya kupiga ramli, na kiburi ni sawa na uovu na kuabudu vinyago. Kwa sababu umeikataa amri ya Mwenyezi-Mungu, naye amekukataa kuwa mfalme.”
Chunguza 1 Samueli 15:23
3
1 Samueli 15:29
Na Mungu ambaye ni utukufu wa Israeli hadanganyi, wala habadili wazo lake. Yeye si binadamu hata abadili mawazo.”
Chunguza 1 Samueli 15:29
4
1 Samueli 15:11
“Ninajuta kwamba nimemfanya Shauli kuwa mfalme. Yeye ameacha kunifuata mimi na hajatimiza amri zangu.” Samueli alikasirika, akamlilia Mwenyezi-Mungu usiku kucha.
Chunguza 1 Samueli 15:11
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video