1
Yohana 15:5
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi. Mtatoa matunda mengi sana mkiwa mmeunganishwa kwangu, nami nimeunganishwa kwenu. Lakini mkitenganishwa mbali nami hamtaweza kufanya jambo lo lote.
Linganisha
Chunguza Yohana 15:5
2
Yohana 15:4
Hivyo mkae mkiwa mmeunganishwa kwangu, nami nitakaa nikiwa nimeunganishwa kwenu. Hakuna tawi linaloweza kuzaa matunda likiwa liko peke yake. Ni lazima liwe limeunganishwa katika mzabibu. Ndivyo ilivyo hata kwenu. Hamwezi kutoa matunda mkiwa peke yenu. Ni lazima muwe mmeunganishwa kwangu.
Chunguza Yohana 15:4
3
Yohana 15:7
Hivyo ninyi mbaki mmeunganishwa nami, na mfuate mafundisho yangu. Mkifanya hivyo, mnaweza kuomba kitu chochote mnachohitaji, nanyi mtapewa.
Chunguza Yohana 15:7
4
Yohana 15:16
Ninyi hamkunichagua mimi. Bali ni mimi niliyewachagua ninyi. Nami niliwapa kazi hii: Kwenda na kutoa matunda; matunda ambayo yatadumu. Ndipo Baba atakapowapa chochote mtakachomwomba katika jina langu.
Chunguza Yohana 15:16
5
Yohana 15:13
Hakuna anayeweza kuonesha pendo lolote kuu zaidi ya kuwa tayari kufa kwa ajili ya rafiki zake. Upendo wa hali ya juu unaoweza kuoneshwa na watu ni kufa badala ya rafiki zao.
Chunguza Yohana 15:13
6
Yohana 15:2
Yeye hulikata kutoka kwangu kila tawi lisilozaa matunda. Pia hupunguza majani katika kila tawi linalozaa matunda ili kuliandaa liweze kuzaa matunda zaidi.
Chunguza Yohana 15:2
7
Yohana 15:12
Hii ndiyo amri yangu kwenu: Mpendane ninyi kwa ninyi kama mimi nilivyowapenda.
Chunguza Yohana 15:12
8
Yohana 15:8
Ninyi mdhihirishe kuwa mmekuwa wafuasi wangu kwa kutoa matunda mengi. Kwani hiyo itamletea Baba utukufu.
Chunguza Yohana 15:8
9
Yohana 15:1
Yesu akasema, “Mimi ndiye mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
Chunguza Yohana 15:1
10
Yohana 15:6
Kama hamtaunganishwa nami, basi mtakuwa sawa na tawi lililotupwa pembeni nanyi mtakauka. Matawi yote yaliyokufa jinsi hiyo hukusanywa, hutupwa katika moto na kuchomwa.
Chunguza Yohana 15:6
11
Yohana 15:11
Nimewaambia haya ili mpate furaha ya kweli kama ile niliyonayo mimi. Nami ninatamani muwe na furaha iliyo kamilifu.
Chunguza Yohana 15:11
12
Yohana 15:10
Nimezitii amri za Baba yangu, naye anaendelea kunipenda. Kwa jinsi hiyo, nami nitaendelea kuwapenda mkizitii amri zangu.
Chunguza Yohana 15:10
13
Yohana 15:17
Hii ndiyo amri yangu: Mpendane ninyi kwa ninyi.
Chunguza Yohana 15:17
14
Yohana 15:19
Kama mngekuwa wa ulimwengu huu, ulimwengu ungewapenda kama watu wake. Lakini ulimwengu unawachukia kwa sababu ninyi siyo wa ulimwengu huu. Badala yake, mimi niliwachagua ninyi ili muwe tofauti na ulimwengu.
Chunguza Yohana 15:19
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video