1
1 Kor 15:58
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Linganisha
Chunguza 1 Kor 15:58
2
1 Kor 15:57
Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Chunguza 1 Kor 15:57
3
1 Kor 15:33
Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
Chunguza 1 Kor 15:33
4
1 Kor 15:10
Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.
Chunguza 1 Kor 15:10
5
1 Kor 15:55-56
Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.
Chunguza 1 Kor 15:55-56
6
1 Kor 15:51-52
Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
Chunguza 1 Kor 15:51-52
7
1 Kor 15:21-22
Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.
Chunguza 1 Kor 15:21-22
8
1 Kor 15:53
Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
Chunguza 1 Kor 15:53
9
1 Kor 15:25-26
Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
Chunguza 1 Kor 15:25-26
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video