1
Warumi 14:17-18
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Kwa maana ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho wa Mungu. Kwa sababu mtu yeyote anayemtumikia Al-Masihi kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na kukubaliwa na wanadamu.
Linganisha
Chunguza Warumi 14:17-18
2
Warumi 14:8
Kama tunaishi, tunaishi kwa Mwenyezi Mungu, nasi pia tukifa tunakufa kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo basi, kama tukiishi au kama tukifa, sisi ni mali ya Mwenyezi Mungu.
Chunguza Warumi 14:8
3
Warumi 14:19
Kwa hiyo na tufanye bidii kutafuta yale yaletayo amani na kujengana sisi kwa sisi.
Chunguza Warumi 14:19
4
Warumi 14:13
Kwa hiyo tusiendelee kuhukumiana. Badala yake mtu aamue kutoweka kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya ndugu mwingine.
Chunguza Warumi 14:13
5
Warumi 14:11-12
Kwa kuwa imeandikwa: “ ‘Kama vile niishivyo,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘kila goti litapigwa mbele zangu, na kila ulimi utakiri kwa Mungu.’ ” Hivyo basi kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa Mungu.
Chunguza Warumi 14:11-12
6
Warumi 14:1
Mkaribisheni yeye ambaye imani yake ni dhaifu, lakini si kwa kugombana na kubishana juu ya mawazo yake.
Chunguza Warumi 14:1
7
Warumi 14:4
Wewe ni nani hata umhukumu mtumishi wa mtu mwingine? Kwa bwana wake tu anasimama au kuanguka. Naye atasimama kwa sababu Bwana anaweza kumsimamisha.
Chunguza Warumi 14:4
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video